AGNESS MASOGANGE KUZIKWA KWAO JIJINI MBEYA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 21 April 2018

AGNESS MASOGANGE KUZIKWA KWAO JIJINI MBEYA.

Video Queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbank kwao jijjni mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.

Akizungumza  dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes  utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders,  na kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi
“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.
Sambamba na  hilo muigizaji Steve Nyerere ambaye yuko karibu na familia ya Agnes amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi leaders jioni ya leo, ili kujadili utaratibu wa mazishi na mengineyo. 
Agnes Masogange amefariki jana April 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pneumonia

No comments:

Post a Comment