ALIKIBA AMEWAANDALIA JAMBO HILI MASHABIKI WAKE. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 27 April 2018

ALIKIBA AMEWAANDALIA JAMBO HILI MASHABIKI WAKE.

Kwa mashabiki wote wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ambao wanapenda kutazama mpira wa miguu au kucheza pia kesho Aprili 27, 2018 ni siku yenu ya kukutana na kufurahi pamoja kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Kidogo Chekundu Kariakoo Jijini Dar es salaam.
Mechi hiyo ya mchezo wa soka itahusisha timu ya mashabiki wa Alikiba (@Teamkiba_football_club) na timu ya mpira wa miguu ya Instagram (@instasokafc).
Tayari Alikiba ametoa baraka zake zote kwa mashabiki wake na kuwataka wahudhurie kwani ni tukio zuri litakalowaunganisha kwa pamoja.
“Instagram Derby:@instasokafc vs @Teamkiba_football_club Hayawi hayawi sasa yamekua Ule wakati tuliokua tukiusubiri sasa umewadia na macho yote yataelekeza katika Viwanja vya JAKAYA KIKWETE Kaskazini mwa Mnazi Mmoja Siku Ya Tarehe 27/4/2018 huku Instasokafc wakiwa kama wenyeji wa mchuano huo.“ameandika Alikiba.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza kesho saa 10:00 jioni na kila mmoja mwenye mapenzi na soka anaalikwa kuhudhuria na hakuna kiingilio.

No comments:

Post a Comment