ZABIBU KIBA BETHIDEI YAKE YAMTOKEA PUANI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 26 March 2018

ZABIBU KIBA BETHIDEI YAKE YAMTOKEA PUANI.

PATI ya bethidei ya dada wa staa wa Afro-Pop, Ali Kiba, Zabibu Kiba aliyofanya juzikati imemtokea puani baada ya kukwaa ugonjwa wa kumlaza kitandani.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Zabibu alisema kuwa, wageni waalikwa waliohudhuria kwenye bethidei yake walimmwagia maji mengi bila kupumzika ambayo yalimsababishia ugonjwa wa kifua na kwenda hospitali kuchomwa sindano kutokana na maumivu kuwa makali.

“Unajua baada ya kumwagiwa maji vile, usiku sikuweza kulala kabisa kwa sababu nilibanwa na kifua mno, ilibidi niende hospitalini kuchomwa sindano ili kipoe ndiyo nikapata nafuu kidogo,” alisema Zabibu.

No comments:

Post a Comment