ZIKIWA zimepita wiki mbili tangu aachie video ya ngoma yake ya Wayu Wayu, mkali wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amekanusha tetesi zilizoenea kuwa aliwaogopa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)ndiyo maana akaigiza kama ‘video queen’ katika video hiyo.
Akizungumza , Dogo Janja alisema, anashangazwa na watu kuendelea kuongelea sababu za kujifanya mwanamke katika video hiyo huku wakihusisha na Basata, alisema alichokifanya ni sehemu ya kazi za sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
“Hapana, siyo kwamba niliogopa Basata, ujue hauwezi kuwa mwanasanaa kama huwezi kuichezea sanaa, nilichofanya ni ubunifu tu,” alisema Dogo Janja.
Katika video hiyo, Dogo Janjaanaonekana akiwa amejipodoa huku akiwa ndani ya mavazi ya kike mwanzo mwisho.
No comments:
Post a Comment