MO MUSIC AIBUKA NA POVU HILI KWA WANAOSEMA KAPOTEA KIMUZIKI . - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 23 March 2018

MO MUSIC AIBUKA NA POVU HILI KWA WANAOSEMA KAPOTEA KIMUZIKI .

BAADA ya madai kuenea kuwa staa wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amepotea kimuziki, ameibuka na kutoa povu si la nchi hii.

Awali, tetesi zilienea kuwa, staa huyo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Basi Nenda kisha Skendo, kwa sasa ameamua kuupa muziki kisogo kutokana na ushindani uliopo na kwamba ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali wa kufuga kuku.

Ilielezwa kuwa, ngoma yake ya mwisho aliyoitoa ya Kibajaj akimshirikisha Roma Mkatoliki ndiyo ‘ilimkata maini kabisa’ baada ya kubuma sokoni.

Showbiz juzikati lilifanikiwa kumuibua Mo Music ambapo lilikutana naye uso kwa uso na kumpelekea madai hayo ya kupotea.

Showbiz: Mambo! Kuna madai yapo kuwa umepotea kimuziki na sasa umejiingiza katika ujasiriamali wa kuku?

Mo Music: Mimi? Nimepotea kivipi? Mbona ngoma zangu zinapigwa redioni? Hata nikifuga hao kuku unaosema cha ajabu kipo wapi?

Showbiz: Lakini madai yanasema Wimbo wa Kibajaj ulivyobuma ndiyo umekufanya kuachana na muziki?

Mo Music: Ninavyojua mimi Kibajaj imefanya vizuri tu, siwezi kupotea na gemu kwangu naliona changa, hao wanaoeneza maneno yote hayo waendelee na umbea wao na ole wake nije kumgundua anayesa-mbaza yote haya!

No comments:

Post a Comment