Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Jijini Mbeya aliyejulikana kwa jina la Idd David kwa tuhuma za kjihusisha na kilimo cha bangi zaidi ya heka mbili katika shamba lake la mahindi kinyume cha sheria za nchi.
Akithibitisha kushikiliwa kwa Mtuhimiwa huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema wamefanikisha kumkamata kutokana na taarifa walizopewa na raia wema kuwa katika eneo Ntantu kata ya Isalaga kuna mtu anajihusisha na kilimo cha Bangi.
Kamanda Mpinga amesema kwa sasa wanaendelea na operesheni maalum ya kudhibiti madawa ya kulevya ikiwemo kilimo cha bangi hivyo kuwataka wakulima wote wanaolima zao hilo wang'oe wenyewe kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment