Shamsa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake kijamii asubuhi ya leo baada ya kupita takribani siku kadhaa tokea kuibuka kwa mjadala mzito mitandaoni kwa kile kilichoonekana kwamba ma-star wa bongo kwa sasa hawana thamani nchini na kupelekea mtu wa kigeni kupewa ubalozi wa jambo fulani ndani ya nchi ambayo yeye haishi.
"Kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikague wenyewe kwanza, nina uhakika kila biashara ina 'condition' zake na kila biashara inahitaji faida. Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua 'star' wa bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara, tusipinge ukweli sisi wenyewe baadhi ya wasanii tumevunja uaminifu kwa wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu", amesema Shamsa.
Pamoja na hayo, Shamsa ameendelea kwa kusema "unapozungumzia kuwa 'ambassador' unazungumzia kubeba 'brand' ya mtu, sasa ni nani anayetaka kuchafua 'brand' yake ibebwe na mtu asiyeeleweka, suala sio kujulikana tu ila unajulikana vipi? maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika. Kikubwa tujifunze, tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika".
Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amesema kulingana na maisha na karne ya sasa ni muhimu kuambiana ukweli ili kuweza kutengeneza mazingira mazuri ya vizazi vya baadae.
No comments:
Post a Comment