MESSI AFUNGUKA MATATIZO YAKE NA DYABALA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 27 March 2018

MESSI AFUNGUKA MATATIZO YAKE NA DYABALA

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amesema hana tatizo na nyota mwenzake wa timu hiyo bali wameshawahi kuongea kuhusu matatizo ya uwanjani na anafahamu wanacheza nafasi moja.

Dybala amewahi kukiri kuwa inamuwia ugumu kucheza pamoja na nyota wa Barcelona na mshindi mara tano wa Ballon d'Or  Lionel Messi kutokana na majukumu yao uwanjani kufanana.

"Mimi na Paul tulizungumza juu ya hilo, kile alichosema ni kweli mana ndani ya Juventus anafanya jukumu sawa na ninalofanya mimi nikiwa Barcelona hivyo tukikutana timu ya taifa lazima mmoja atapata ugumu lakini tuko sawa na tunajitahidi kwaajili ya taifa," amesema Messi.

Messi ameongeza kuwa anafahamu kwanini Dybla amesema hivyo kwasababu anapata taabu sana kucheza katika eneo la kushoto kwenye timu ya taifa kitu ambacho hata yeye huwa anakipitia na hufurahia zaidi kucheza katikati ya uwanja na kutokea kulia kuingia ndani.

Messi anatarajia kuanza leo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania utakaopigwa kwenye dimba la Wanda Metropolitano jijini Madrid baada ya kukosa mechi dhidi ya Italy ambapo timu yake ilishinda 2-0.

No comments:

Post a Comment