MNAWAFUNGIA DIAMOND,ROMA MTAIMBA NYIE..: KHERI JAMES - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 27 March 2018

MNAWAFUNGIA DIAMOND,ROMA MTAIMBA NYIE..: KHERI JAMES

Kufuatia sakata la kufungiwa kwa baadhi ya wasanii na nyimbo zao, akiwemo Roma Mkatoliki, Diamond Platnumz, Snura na wengine, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James, amekerwa na maamuzi hayo yaliyofanywa na Basata na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kupitia kwa Naibu wake, Juliana Shonza.

Akizungumza jana Mjini Dodoma, Kheri James alieleza masikitiko yake na kusema kuwa wizara hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya wasanii ambao wengi wao ni vijana wanaojitafutia kipato kupitia tasnia hiyo.

“Mmemfungia Roma, mmemfungia Diamond na wengine, kila anaenyanyuka mamkata mguu, hivi mnavyowafungia mtaimba nyie?

“Kama wizara itendelea na tabia hiyo ya kuwafungia wasanii, na wao ndio viongozi wa sanaa je watamsimamia nani wakishawafungia wote?” alihoji Kheri.

No comments:

Post a Comment