Nuh Mziwanda afunguka ya moyoni baada ya nyimbo yake kuvuja - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 7 February 2018

Nuh Mziwanda afunguka ya moyoni baada ya nyimbo yake kuvuja

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amejikuta akihuzunishwa na kitendo cha wimbo wake kuvuja kwani hakuwa na mpango wa kuutoa sasa hivi.

Akipiga story Nuh alisema wimbo huo unaojulikana kwa jina la Upofu ulivuja hivi karibuni huko mkoani Morogoro baada ya mdogo wake kwenda na flash iliyokuwa na wimbo huo kwenye kibanda cha kuingiza nyimbo kuweka nyimbo na hapo ndipo ulipochukuliwa kwenye flash na kuanza kupigwa.

“Nimeumia sana maana wimbo huo haukuwa kwenye mpango wa kuutoa sasa hivi lakini ndiyo hivyo imeshatokea umevuja, nawaomba mashabiki zangu waupokee na wanipe sapoti ili kuweza kusonga mbele zaidi kimuziki ndani na nje ya nchi,” alisema Nuh Mziwanda.

No comments:

Post a Comment