Lulu Diva akanusha haya kumuhusu mpenzi wake.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 6 February 2018

Lulu Diva akanusha haya kumuhusu mpenzi wake..

Msanii wa kike wa muziki bongo Lulu Diva amefunguka tuhuma za kuachwa na mpenzi wake wa muda mrefu, na kunyang'anywa vitu ambavyo alimnunulia.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv , Lulu Diva amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, ingawa ni kweli kulitokea kutoelewana na mpenzi wake kutokana na msanii anayejulikana kwa jina la Richad, lakiini ana amini yatakwisha na wataelewana.

“Ni vitu ambavyo vimetokea lakini siwezi kuviongelea sana, ila nikwamba jamaa siko kwenye mahusiano naye, kwa hiyo mpenzi wangu vimekuwa kwake ni tofauti kuolewa lakini I hope soon tutakaa sawa, kuhusu kunyang'anywa vitu sio kweli sijanyang'anywa na hawezi kufanya hivyo, ilikuwa tu ni ugomvi”, amesema Lulu Diva

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva yupo kwenye mahusiano na msanii moja hapa bongo kiasi cha kuvuja kwa picha wakiwa kwenye pozi za mahaba, kitendo ambacho kimeonekana kumchukiza mpenzi wake wa siku nyingi ambaye hajulikani kabisa mitandaoni.

No comments:

Post a Comment