Mimi Mars afunguka mahusiano yake na Jux.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 7 February 2018

Mimi Mars afunguka mahusiano yake na Jux..

 MIMI Mars ni miongoni mwa wanadada wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva. Jina lake alilopewa na wazazi wake ni Marianne Mdee na ni mdogo wa damu wa mwanamuziki Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Mbali na kuwa mwanamuziki, Mimi Mars ambaye hana muda mrefu kwenye gemu lakini akiwa na nyimbo kali zikiwemo Nadata, Shuga na wimbo mpya wa Sitamani, pia ni mtangazaji wa televisheni.

Katika makala haya Mimi Mars amefunguka mambo mengi kuhusu muziki wake pamoja na maisha binafsi.

Risasi Vibes: Ujio wako mpya mapokezi yake yamekuwaje?

Mimi Mars: Ukweli ni kwamba mapokezi yamekuwa mazuri, wimbo umefanya vizuri ndani na nje ya Bongo na hata idadi ya watu wanaonisapoti wameongezeka kiukweli.

Risasi Vibes: Kwa uonavyo wewe, nani ni mshindani wako kwenye muziki Bongo?

Mimi Mars: Kiukweli sina mshindani, kila mwanamuziki anafanya muziki kwa namna yake mwenyewe, kwa hiyo mshindani wangu naweza kusema ni mimi mwenyewe. Nashindana kila siku ili kuleta mvuto zaidi kwenye kazi zangu.

Risasi Vibes: Mwanamuziki gani wa kike anakuvutia na ambaye unapenda kufanya naye kazi ndani na nje ya Bongo?

Mimi Mars: Kiukweli wanamuziki wanaonivutia ni wengi ndani na nje ya Bongo. Lakini sana ningependa kufanya kazi na wanamuziki wa nje ya nchi wakiwemo Yemi Alade, Seyi Shay, Tiwa Savage, Niniola, Fena, Victoria Kimani, kiukweli listi ipo ndefu sana.

No comments:

Post a Comment