Siri yafichuka..Ngoma ya kivuruge ya Nandy.... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 6 February 2018

Siri yafichuka..Ngoma ya kivuruge ya Nandy....

IMEFICHUKA! Ile Ngoma ya Kivuruge iliyoimbwa na msanii zao la Jumba la Kuibua Vipaji ‘THT’, Faustina Charles ‘Nandy’ kumbe ilishawahi kuimbwa na msanii kutoka THT, Juma Said ‘Jay Melody’.

Akizungumza Jay Melody ambaye anatamba na Wimbo wa Goroka ambao upo namba mbili katika chati za Top 20, Clouds FM alisema, alifuatwa na Nandy baada ya kuutoa Wimbo wa Kivuruge na kuomba aurudie.

“Nandy alinifuata baada ya kusikia nimeutoa, akaniomba kuurudia basi tukakubaliana na uongozi wake nikampatia, kwa hiyo ni mimi ndiye niliutunga na hakuna hata mstari uliobadilika,” alisema Jay Melody.

Full Shangwe ilimtafuta Nandy kujua ukweli juu ya wimbo huo ambapo alisema;

“Ni kweli uliimbwa na Jay Melody na kuna makubaliano tuliyafikia ndiyo nikaurudia.”

Nandy pia anatamba na vibao kadhaa vikiwemo One Day, Nagusa Gusa na Wasikudanganye.

No comments:

Post a Comment