Idriss afunguka anacho kiogopa kuhusu wanawake... - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 8 February 2018

Idriss afunguka anacho kiogopa kuhusu wanawake...

Mfanyabiashara na mchekeshaji maarufu bongo Idriss Sultani amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake ya sasa anaogopa sana wanawake wa jamaa zake pamoja na wake za watu na kuwa hawezi kujitoa ufahamu na kupita nao.

Idris aliweka bayana hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI LIVE kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi kamili jioni.

"Siku hizi kusema kweli naogopa sana wake za watu maana ukishaona mtu amenyolewa kipara kinachofuata kiukweli si kizuri, sijawahi kutoka na mke wa mtu na sijui kama imeshawahi kutokea hivyo ila nachojua mimi sitataka kusikia mtu ametoka na mke wangu halafu kesho yake kusiwe hata na msiba kwao au kwangu, lazima kuwe na namna ya kuadabishana kwa mambo madogo madogo kama hayo yaani umetoka na mke wangu na mimi natoka na maisha yako. Kwa hiyo mimi siwezi kugusa mke wa mtu kwa sababu sitaki mke wangu aguswe" alisisitiza Idris

Idris aliendelea kusema kuwa mbali ya wake za watu kwake yeye hajisikii poa pia kutoka kimapenzi na wanawake au mabinti wa karibu na rafiki zake

"'Girlfriend' ni vitu vya kupita ni sawa na kikombe na sahani kila mtu anaweza kukitumia labda mtu awe amefanya 'commitement' na kumchukua kuwa mke hapo sasa tunaongea lugha nyinge ila katika vitu pia naogopa kuliko vyote ni ma 'Girlfriend' wa masela zangu kabisaa nawaogopa sana" alisisitiza Idris Sultan.

No comments:

Post a Comment