Simba yambana Liuzio - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 28 November 2017

Simba yambana Liuzio

HARAKATI za klabu ya Singida United ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi hawataki kumuachia.

Singida inamuhitaji Liuzio kwa ajili ya kuongezea nguvu kikosi chake kwenye mzunguko wa pili baada ya kurizishwa na kiwango chake.

Rafiki wa karibu wa Liuzio amesema, ni kweli Singida wanamuhitaji mchezaji huyo lakini Simba imeonyesha dalili zote kuwa haitaki kumuachia.

"Kweli Singida inamtaka, Liuzio lakini Simba wamegoma, hawataki kumtoa sasa sijui kwa nini wakati
wenyewe hawampi nafasi kubwa ya kucheza. Bora wangemtoa akajaribu maisha mengine huko,"alisema.

Liuzio mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, klabu iliyomlea na kumuuza Zesco ya Zambia, alirudi nchini mwaka jana akasajiliwa kwa mkopo na Simba anayoichezea mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment