Simba kumpoteza Liuzio - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Simba kumpoteza Liuzio

Mshambuliaji wa Simba, Juma Liuzio amechoka kusugua benchi katika timu hiyo na sasa anataka kuvunja mkataba wake na kutimkia Singida United ambao wameonyesha nia ya kusajili wakati huu wa dirisha dogo.

Liuzio sio chaguo la kwanza la kocha Joseph Omog na badala yake amekuwa akianzia benchi jambo ambalo linaonekana halinfurahishi kwani anaamini ana uwezo mkubwa wa kupambana katika kikosi cha kwanza hivyo anaona kipaji chake kinazidi kupotea.

Hivyo Luizio ameona ni vyema aondoke akamalizie soka Singida United kabla hajaanza kufanya mchakato wake wa kwenda kucheza soka la kulipwa.

"Kiwango changu hakijashuka ila mfumo anaotumia kocha sio rafiki kwangu ndiyo maana naona ni vyema niende kucheza sehemu ingine kwani lengo langu kama mchezaji ni kucheza na sio kukaa benchi. 

Kukaa benchi kutaendelea kunipoteza hivyo naamini viongozi wangu watakubaliana na mimi kuondoka Simba.
"Kikubwa ninachohitaji wanikubalie kuvunja mkataba nisiwadai nao wasinidai lakini sio kuondoka kwa mkopo, tayari kuna mazungumzo ambayo yanaendelea na viongozi wa Singida United ambayo naamini yatakwenda vizuri, mpira ni kazi yangu kukaa benchi hakutanisaidia," alisema Liuzio.

No comments:

Post a Comment