Yanga kumchukulia hatua kali Donald Ngoma - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 15 November 2017

Yanga kumchukulia hatua kali Donald Ngoma

STRAIKA wa Yanga, Donaldo Ngoma alitarajiwa kutua nchini jana akitokea kwao Zimbabwe, lakini uongozi wa klabu yake umepanga kumchukulia hatua kali kama atatoa majibu yasiyoridhisha. Ngoma alipewa ruhusa ya kwenda Zimbabwe kwa mapumziko madogo kutokana na kuwa majeruhi, lakini alikaa huko zaidi ya muda aliopewa bila kutoa taarifa. Kutokana na hilo, mabosi wake wamepanga atakapofika tu aeleze kilichomfanya achelewe na kama atatoa majibu yasiyoridhisha, atachukuliwa hatua kali. Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema: "Taarifa ya kurudi kwake ilikuwa jana na atakapofika, atatakiwa aeleze kilichomchelewesha na kama hatakuwa na sababu zisizo na mashiko, itabidi ahadhibiwe. Amepewa muda wa kujieleza kwa sababu yeye ni binadam, huenda alikuwa na sababu zenye mashiko.” Ngoma alipata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wao na Mtibwa Sugar jijini Dar es Salaam, maumivu hayoyaliyomweka nje ya uwanja akakosa mechi nne za ligi ikiwemo ya watani wao Simba. Hata hivyo, inadaiwa mchezaji huyo yuko mbioni kujiunga na Singida United inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Mholanzi Hans Pluijm.

No comments:

Post a Comment