Mil 178 itapendeza - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Mil 178 itapendeza

HABARI mpya ni kwamba yule winga wa Simba ambaye hana masihara kabisa na Yanga, Shiza Kichuya, amegoma kusaini mkataba mpya klabuni hapo baada ya kupata ofa ya maana kutoka kwa timu moja ya Uarabuni.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji kadhaa ambao mikataba yao na Simba inaelekea ukingoni na mabosi wa timu hiyo tayari wameanza kuhaha kumshawishi auongeze na Meneja wake ambaye ni Profesa Midundo Mtambo amefafanua.

Profesa Midundo amesema kuwa mbali na hilo wameangalia ofa ambayo nyota huyo amepewa ya dola 80,000 (Sh177 milioni) kuwa ni kubwa kuliko ambayo atapewa na Simba.

“Atakwenda Misri, ni kwenye timu ile ile iliyokuwa ikimuhitaji mwanzoni ambapo Simba walitaka pesa nyingi hivyo wakashindwa kumalizana, ndiyo maana waliona ni vema amalize mkataba aondoke akiwa mchezaji huru,” alisema.

“Simba inataka kumwongeza mkataba Kichuya, lakini nimewaambia wasubiri kwanza mpaka mkataba wake utakapomalizika hiyo mwakani, hivyo hataongeza kwa sasa, kikubwa tunaangalia hiyo ofa labda Simba waje na ofa nzuri zaidi napo pamoja na ofa yao mchezaji hataweza kusaini kwa sasa.”

Profesa Midundo alisema kuwa wachezaji wote anaowasimamia wanaoichezea Simba akiwemo Yassin Mzamiru wapo huru kuzungumza na timu nyingine kwa sasa kwani mikataba yao inamalizika.

“Hata Mzamiru mkataba wake unamalizika na tupo tayari kuzungumza na timu yoyote ambayo itamuhitaji. Hatutaki asaini kwanza Simba hadi amalize kabisa mkataba huu wa sasa,” alisema kusema meneja huyo.

No comments:

Post a Comment