ALIKIBA NAOMBA WAHURUMIE : OMMY DIMPOZ - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 3 May 2018

ALIKIBA NAOMBA WAHURUMIE : OMMY DIMPOZ

Msanii Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake 'yange' ambao ameshirikiana na msanii Seyi Shay kutokea nchini Nigeria, amemuomba msanii Alikiba awahurumie.

Ommy Dimpoz alisema hayo baada ya Alikiba kutangaza rasmi kuwa wimbo huo mpya wa Ommy Dimpoz ukifikisha watazamaji milioni tatu Youtube basi na yeye ataamsha dude na kuachia wimbo wake mpya baada ya 'Seduce Me' ambayo iliachiwa mwaka jana mwezi Agosti. 
Baada ya ahadi hiyo ya Alikiba ndipo alipokuja Ommy Dimpoz na kumuuliza Alikiba kama atatoa ngoma zote tano kwa wakati mmoja au ataanza kuachia moja moja, hii ni ishara kwamba tayari kuna nyimbo zaidi ya tano kutoka wa Alikiba ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa. 
Aidha Msanii Alikiba akijibu moja ya swali kutoka kwa shabiki yake kupitia mtandao wa jamii ambaye alitaka kufahamu kuwa hilo dude ataliamsha lini ndipo alipojibu kuwa anawapa siku 10 tu baada ya hapo anaweza kuachia wimbo wake huo mpya

No comments:

Post a Comment