Tambwe ahamisha namba ya Tshishimbi - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Tambwe ahamisha namba ya Tshishimbi

STRAIKA mwenye rekodi bora ya kucheka na nyavu katika kikosi cha Yanga, Amissi Tambwe, amerudi mzigoni na ana siku ya tatu sasa mazoezini.

Tambwe ametamka kwamba endapo Thabaan Kamusoko angekuwa sawa na kupewa na majukumu ya kiungo mkabaji huku Papy Tshishimbi akisogezwa juu, huo utakuwa mtaji mkubwa kwake na washambuliaji wenzake kutupia.

“Nashukuru sasa najisikia tofauti tangu nimeanza mazoezi nafikiri kama mambo yakiendelea hivi basi hakuna shaka nitarudi kuungana na wenzangu kuisaidia timu nilikuwa naumia timu inapokosa mchango wangu,”alisema Tambwe.

“Muda wote niliokuwa nje kama kuna kitu nilikuwa nakikosa na kinaniumiza basi ni kutocheza pamoja na Tshishimbi, nakumbuka alikuja tukiwa Pemba na baada ya hapo nikaumia siku zile chache zilitosha kwangu kugundua jamaa ni mchezaji hatari.

“Kama ningekuwa na uwezo ningemuomba kocha ampange kama kiungo mchezeshaji namuona kama Tshishimbi angekuwa na nafasi bora zaidi ya kutupa mipira ya kutosha kutokana na uwezo wake ni vile Kamusoko bado mgonjwa, tungefunga sana,” anasisitiza Tambwe ambaye aliwahi pia kucheza Simba kwa mafanikio.

No comments:

Post a Comment