Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mama yake, Lucresia Kalugira (kulia).
MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Kalugira, kwa kipindi kigumu alichokianza jana baada ya bintiye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Lulu akiwa na Idris.
Sultan amesema jamii impe faraja na kumtia moyo wakati akiwa katika huzuni ya kuwa mbali na binti yake. Pia Sultan amemuelezea Lulu kuwa alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ni mwanamke shupavu ambaye huzuni yake ikiwa jela itachukua muda mfupi kabla ya kupata marafiki na kujipa moyo wa kuhimili maisha hayo mapya ya miaka miwili.
Hayo ni maneno aliyoyatuma kwenye akaunti yake ya Instagram kama yafuatavyo:
My last piece on this, Mama Lulu tunakuombea kwa Allah upate nguvu ya kukubaliana na hii hali ambayo ni chungu kwetu sote. Tunalazimika kukubali kwasababu Mungu tu ndiye anajua kubaki na jambo kama hili moyoni kwa mda mrefu hivi linaondoaje amani. Binafsi nampenda sana Lulu na anajua, kwa mda wa miaka michache niliyojuana na Liz najua wewe mama ndio tunahitaji kukuangalia zaidi maana Lulu najua atalia wiki ya kwanza na ya pili, ya tatu atapata kazi jikoni, ya nne anajisomea, ya tano kashapata marafiki kote because your daughter is the strongest woman I have ever met maishani mwangu yani ningekua mwanamke ningekua yeye.
Baby is good to go na nitajaribu kuwa positive na kusema kua ntammiss sana ila mara mbili tatu sitoacha kumtembelea na tunasubiri siku anatoka na ku-take over her throne. Hakuna aliyependa haya yatokee ila ndio yametokea we only have God and each other now. Be blessed
No comments:
Post a Comment