Idris Sultan afunguka haya kuhusu maisha ya kanumba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 14 November 2017

Idris Sultan afunguka haya kuhusu maisha ya kanumba

Mcheeshaji na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan.

MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, na kuelezea alivyoyakumbuka maisha mema ya Kanumba wakati akiwa hai duniani na kuongeza kwamba sasa haki yake imepatikana baada ya hukumu kutolewa na Mahakama Kuu na anatumaini atapumzika kwa amani milele.

Marehemu Kanumba. Huu ndiyo ujumbe aliouandika kupitia akaunti yake ya Instagram: Najua ulikua hunijui ila nilitembea kwa miguu kutoka mbezi kimara mpaka kinondoni kuja kukuzika. Ni mda mrefu sana umekua ukitembea na sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzika kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki mioyoni mwetu. Tulifunga njia, kazi na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na tukapata depression kubwa sanaaaa yote kwasababu ulitugusa katika mfano usioelezeka.

 Naamini haki yako sasa imepatikana na namuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo. Finally Rested. Ni mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan

No comments:

Post a Comment