Sekunde ya mwisho Chelsea yaibuka na ushindi wa bao 2-1 dhiidi ya Atletico Ugenini - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 27 September 2017

Sekunde ya mwisho Chelsea yaibuka na ushindi wa bao 2-1 dhiidi ya Atletico Ugenini

Mabingwa wa Uingereza, Klabu ya Chelsea wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid kwenye usiku wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Mechi hiyo ya mzunguko wa pili hatua ya makundi ilipigwa kwenye dimba jipya la Atletico Madrid la Wada Metropolitano mbele ya mshambuliaji Diego Costa ambaye alikuwa jukwaani kushuhudia mchezo huo.

Michy Batshuayi aliibuka shujaa baada ya kutokea benchi na kufunga bao la ushindi sekunde ya mwisho kabla ya mchezo kumalizika akimalizia vyema pasi ya Marcos Alonso.

Atletico Madrid walikuwa wa kwanza kuandika bao kwenye mchezo huo uliowakutanisha makocha wawili machachari, Diego Simeone kwa upande wa Atletico na Antonio Conte kwa upande wa Chelsea.

Griezmann aliandika bao hilo dakika ya 40 kwa mkwaju wa penati baada ya David Luiz kumwangusha mchezaji wa Atletico kwenye eneo la hatari wakati wa harakati za kuzuia mpira wa kona huku Chelsea wakisawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Alvaro Morata aliyeweka mpira kimiani kwa kichwa akiunganisha krosi murua iliyochongwa naye Eden Hazard.

Kwa matokeo hayo sasa Chelsea wanafikisha alama sita na kuongoza kundi C baada ya kushinda michezo miwili akifuatiwa na AS Roma mwenye alama tatu ambaye aliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Qarabag kwenye mchezo uliopigwa mapema, Atletico katika nafasi ya tatu akiwa na alama moja huku Qarabag akiburuza mkia bila ya alama yoyote.

No comments:

Post a Comment