KUANZIA leo Ijumaa, zitakuwa zimesalia siku 20 kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka huu ambayo itakayofanyika nchini Urusi ambapo tunatarajia kushuhudia burudani za kila aina kutoka kwa wachezaji maarufu wanaoziwakilisha timu zao za taifa.
Wakati tukitarajia kushuhudia burudani hiyo, jambo la kujivunia ni kwamba Tanzania licha ya kutokuwa na timu itakayotuwakilisha, lakini kupitia muziki, tutawakilishwa ambapo msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, atatumbuiza katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Kupitia Wimbo wa Colours, Diamond atatumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi ambapo wimbo huo ndiyo maalum kwa fainali za mwaka huu.
Akiwa na msanii kutoka Marekani, Jason Derulo, Diamond anatarajia kuipeperusha vema bendera ya Tanzania Juni 14 katika Uwanja wa Luzhniki ambao unachukua watazamaji 81,000 kwa wakati mmoja.
Wakati tukitarajia kushuhudia burudani hiyo, jambo la kujivunia ni kwamba Tanzania licha ya kutokuwa na timu itakayotuwakilisha, lakini kupitia muziki, tutawakilishwa ambapo msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, atatumbuiza katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Kupitia Wimbo wa Colours, Diamond atatumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi ambapo wimbo huo ndiyo maalum kwa fainali za mwaka huu.
Akiwa na msanii kutoka Marekani, Jason Derulo, Diamond anatarajiwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania Juni 14 katika Uwanja wa Luzhniki ambao unachukua watazamaji 81,000 kwa wakati mmoja.
Siku zote watu wanasema michezo huwakutanisha watu wa aina mbali mbali, maadui , marafiki na hata wenye rika tofauti. Hilo pia kwamba wote watakuwa sehemu moja wakifanya jambo fulani, hapana, bali kila mmoja kupitia nafasi yake, atajumuika na wapenda soka duniani kote kuwa kwenye familia moja ya soka.
Wakati Diamond akiwa mtumbuizaji kwenye sherehe za ufunguzi, mwenzake Alikiba kupitia kinywaji cha Mofaya, atakuwa mdhamini wa michuano hiyo ambayo itakuwa ikionyeshwa na chaneli za hapa nyumbani za TBC 1 na TV1.
Hivi karibuni, Alikiba alisema: “Kama shabiki wa soka, nina furaha kujihusisha na michuano ya Fifa World Cup Russia 2018. Safari hii tunaungana pamoja bila kujali umri, dini wala jinsia katika kushabikia michuano hii na ninajivunia kwamba Mofaya Energy Drink inatoa sapoti kufanikisha suala hili.
“Ningependa kuwashukuru TV1 na TBC 1 pamoja na wadhamini wenzangu katika kuhakikisha Watanzania wote wanapata nafasi ya kuangalia Fifa World Cup.“Tusepe Russia na Mofaya Energy Drink kupitia TBC 1 na TV1 kuangalia michuano mikubwa kabisa ya soka duniani.”
Naye Diamond wakati amepewa dili la kutumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi, amesema: “Ukiniuliza hata sijui ni nini hasa waliangalia hadi kuniona mimi, lakini ghafla tu nilishangaa kuona simu, naambiwa nimeteuliwa.” Ikumbukwe kuwa, michuano ya mwaka huu ni ya 21 kufanyika tangu ilipoanzishwa miaka 88 iliyopita.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Ujerumani ambapo imeutwaa ubingwa huo mwaka 2014 wakati fainali hizo zilipofanyika nchini Brazil. Historia ya michuano hiyo inaonyesha kwamba, Brazil ndiyo imelichukua taji hilo mara nyingi kuliko mataifa mengine. Imelichukua mara tano, ikifuatiwa na Ujerumani na Italia zilizochukua mara nne kila moja.
No comments:
Post a Comment