Baada ya kufunga mabao mawili wakati Simba ikiitwanga MWadui FC kwa mabao 3-0, Emmanuel Okwi amesema pamoja na juhudi, ushirikiano na wenzake ndiyo chachu ya mafanikio hayo.
Okwi raia wa Uganda amesema ushirikiano wake na wenzake umemfanya kufikisha mabao 6 katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara.
“Ushirikiano na wenzangu ndiyo jambo namba moja zaidi, nimefanikiwa kufunga mabao mawili na kufikisha sita kwa kuwa tunashirikiana na wenzangu, nawashukuru.
“Kingine ni juhudi lakini pia kumuamini Mungu kutokana na ninachokitaka,” alisema.
Katika mechi ya kwanza ambayo Simba ilishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ambayo ilikuwa ya ufunguzi wa ligi, Okwi alifunga mabao manne.
Katika mechi ya pili, hakucheza wakati Simba ikitulizwa kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC.
No comments:
Post a Comment