FULL TIME SIMBA 3-0 MWADUI KUTOKEA UWANJA WA UHURU. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 17 September 2017

FULL TIME SIMBA 3-0 MWADUI KUTOKEA UWANJA WA UHURU.


MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 88, Kabunda anawekwa chini hapa, eneo nje kidogo ya lango la Simba. Inachongwa na Ndeule faulo juuuu
Dk 87 Okwi anapiga mkwaju wa adhabu lakini mpira unatoka nje sentimeta chache
KADI Dk 86, Seseme analambwa kadi ya njano kwa kumkatwa mtama Kotei
Dk 84, Okwi tena anawachambua mabeki wa Mwadui FC, anaachia mkwaju unambabatiza beki na kuokolewa
Dk 82, Okwi anajaribu kumtoka Mfuko hapa anatoa na kuwa kona, inachongwa, MWadui FC wanaokoa
Dk 80 sasa, tunakwenda dakika 10 za mwisho na Simba wanaendelea kutawala mchezo hasa sehemu ya katikati
Dk 78, Malika Ndeule anaachia mkwaju mkali kabisa, lakini Manula anadaka kwa ustadi mkubwa
SUB Dk 77, Jonas Mkude anaingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude
Dk 75, Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Kabunda
Dk 73, nafasi nzuri kwa Simba, Okwi anatoa pasi nzuri kwa Okwi lakini shuti lake halikulenga lango, goal kick
GOOOOOOOO Dk 72, Bocco anamchambua beki na kufunga bao safi la tatu kwa Simba na la kwanza kwake
Dk 70 Okwi anaachia mpira wa adhabu hapa, unatoka sentimeta chache kabisa
SUB Dk 70, Awadhi Juma ambaye ni nahodha wa MWadui anakwenda nje, Awesu Ally anachukua nafasi yake
Dk 69, Bocco anaangushwa nje kidogo ya lango la Mwadui akiwa anawatoka mabeki
GOOOOOOOOO Dk 67 Okwi anachukua anatisha, anaachia mkwaju mkali na kuandika bao safi kabisa
Dk 66, krosi safi ya mpira wa adhabu, Juuko anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick
SUB Dk 65, Kichuya anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Laudi Mavugo
KADI Dk 65 Mfuko analambwa kadi ya njano baada ya kuzozana na mwamuzi
Dk 63, Mwadui FC wanagongeana vizuri, Awadhi anaachia shuti kali lakini linapaaa juuuu
SUB Dk 60, Mwinyi Kazimoto anaingia upande wa Simba kuchukua nafasi ya Gyan
Dk 58, Mbonde anaruka na kuondosha mpira inachongwa hapa, shuti linapigwa lakini Manula anadaka
Dk 56, MWadui wanafanya shambulizi hapa na kupata kona, mpira unachongwa na Manula anadaka kwa ustadi mkubwa
Dk 54, Simba wanagongeana vizuri, Bocco anakuwa wa mwisho, anaachia mkwaju, kona. Inachongwa vizuri na Kichuya Mwadui wanaokoa
Dk 52 Manula analazimika kuruka juu kudaka mpira wa krosi wa Ndeule
Dk 51, Okwi anaingia vizuri, anabaki yeye na kipa Massawe anaachia mkwaju mkali kipa anadaka hapa
Dk 48, Okwi anaingia vizuri, anatoa krosi nzuri lakini Ndeule anaokoa vizuri kabisa
Dk 45 Simba wameanza kwa kasi wanaonekana wamepania kupata bao la pili
MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa lakini beki anazuia na kipa anauwahi
Dk 44, mpira zaidi unachezwa katikati ua uwanja
Dk 42, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa kupitia Gyan ambaye anaonyesha hayuko siriaz
Dk 39, mpira wa adhabu unatua kichwani kwa Kotei lakini anapiga juuuuuu, goal kick
SUB Dk 35 Gerrard Mathias anakwenda nje kwa MWadui, wanamuingiza Benedicto Mwampyate
Dk 30 Okwi anaingia vizuri, mpira unaokolewa na kuwa kona, inachongwa inaokolewa
Dk 26,Bocco tena anaingia na kupiga krosi safi, inaokolewa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya na kipa anadaka kwa ulaini
Dk 25, Bocco anaruka na kupiga kichwa safi cha kuchupa lakini Massawe anauona
Dk 25, Kichuya anaachia mkwaju mkali unagonga mtambaa wa Panya
Dk 24, pasi nzuri ya Kichuya, Gyan anaachia mkwaju wa chinichini lakini kipa Massawe wa Mwadui anadaka vizuri
Dk 21, mwadui FC wanafanya shambulizi mfululizo na Kabunda anaachia shuti tena, lakini hakulenga lango, goal kick
Dk 20, Mwadui FC wanapata faulo nje kidogo ya lango la Simba, Kabunda aliwekewa kigingi
Dk 19, Awadhi Juma anaachia mkwaju lakini unakuwa nyanya hapa
Dk 16, Okwi anapiga shuti la mkwaju wa faulo lakini mpira unapita juuu
Dk 15, Simba wanapata faulo nje kidogo ya lango la Mwadui FC, Okwi alifanyiwa madhambi.
Dk 12 Seseme naye katika nafasi nzuri lakini mpira wake wa krosi unaishia mikononi mwa Manula
Dk 9, Malika Ndeule anaingia vizuri lakini Juuko anaokoa vizuri
GOOOOOOOOO Dk 7, Okwi anafunga bao baada ya kupiga mkwaju wake uliomgonga beki na kujaa wavuni. Alipokea pasi ya Kichuya aliyegongeana naye vizuri
Dk 5 sasa Simba, wanaonekana kupambana na MWadui FC katikati ya uwanja lakini hakuna mashambulizi
Dk 1, Nicholas Gyan naye anaingia vizuri kabisa na kuachia mkwaju lakini inakuwa ni goal kick
Dk 1, Mwadui FC wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Simba lakini shuti lililopigwa linapita juu
KIKOSI CHA SIMBA:
1. Aishi Manula
2. Ally Shomari
3. Mohamed Zimbwe Jr
4. Salim Mbonde
5. Juuko Murshid
6. James Kotei
7. Nicholous Gyan
8. Muzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya
AKIBA:
Emmanuel Mseja
Jamal Mwambeleko
Jonas Mkude
Said Ndemla
Mwinyi Kazimoto
Laudit Mavugo

No comments:

Post a Comment