kesi ya Lulu kuhusu mauaji ya Kanumba kuanza kusikilizwa rasmi Mahakamani - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 16 October 2017

kesi ya Lulu kuhusu mauaji ya Kanumba kuanza kusikilizwa rasmi Mahakamani

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu October 19, 2017.

Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku hiyo ya October 19, 2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

February 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali (PH) alikiri Mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kuwa kulikuwepo na ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha Mwigizaji huyo.

Lulu aliachiwa kwa dhamana January 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashtaka kutoka kwenye kesi ya mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.

Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa April 7, 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.

No comments:

Post a Comment