Straika wa Yanga, Obrey Chirwa jana Jumanne jioni, aligeuka kuwa bondia baada ya kumshambulia kwa kipigo mpiga picha John Dande wa New Habari kwenye mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Uhuru, ikidaiwa kukerwa kupigwa picha.
Beki Juma Abdul alifanya kazi ya ziada ya kuingilia kati na kumuokoa mpigapicha Dande alijeruhiwa na Mzambia huyo aliyeonekana kuwa na hasira huku pia mkononi akiwa ameshika mkasi wa kukatia nyasi aliotaka kumjeruhi nao Dande.
Tukio hilo limeripotiwa Kituo cha Polisi cha Chang'ombe, huku uongozi wa Yanga ukikaririwa kutofurahishwa na kilichofanywa na nyota wao huyo.
Chanzo cha mkasa huo kinaelezwa na Chirwa alikerwa na Dande baada ya wiki iliyopita kuwapiga picha wakati wa mgomo baridi wa kushinikiza walipwe mishahara yao.
No comments:
Post a Comment