Chelsea wana mpango wa kumuongezea mshahara mchezaji wao nyota, Eden Hazard kufikia paundi 300,000 kwa wiki ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi nchini Uingereza.
Hazard kwa sasa analipwa mshahara wa paundi 220,000 kwa wiki na endapo atafanikiwa kulipwa kiasi hicho cha pesa basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi akiwapiku Paul Pogba na Romelu Lukaku.
Nyota wa Manchester United, Paul Pogba analipwa paundi 290,000 kwa wiki huku Lukaku naye ambaye amejiunga na United dirisha hili la usajili akitokea Everton akishika nafasi ya pili kwa malipo akiwa anachukua mshahara wa paundi 250,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment