Mashabiki acheni ushamba- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 22 September 2017

Mashabiki acheni ushamba- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela amewaambia mashabiki wa soka mkoani kwake waache ushamba wa kuzishangilia timu za mbali zinapokwenda na timu zao za nyumbani.
Mongela ametoa ujumbe huo kupitia account yake ya twitter (@john_mongela) mara baada ya Mbao kupata sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Simba katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa CCM Kirumba September 21, 2017.
“Watu wa Mwanza tuna timu nzuri ya Mbao. Kushabikia timu za mbali ni ushamba, lazima tuache ushamba tujivunie vyetu vya nyumbani. #TeamMbao”-John Mongela.
Mongela alikuwepo uwanja wa CCM Kirumba kuwashuhudia vijana wake wa Mbao wakipambana na Simba

No comments:

Post a Comment