Klabu ya Chelsea imethibitisha kupitia tovuti yake rasmi kuwa imefikia makubaliano na klabu ya Atletico Madrid kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji Diego Costa.
Costa hajacheza kwenye kikosi cha Chelsea tangu mwezi Mei mwaka huu kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Arsenal baada ya kocha Antonio Conte kumtumia ujumbe mfupi akimwambia kuwa hayupo kwenye mipango yake ya msimu ujao.
Uhamisho huo wa Diego Costa utategemea maslahi binafsi kati ya mchezaji na klabu ya Atletico Madrid pamoja na vipimo vya afya.
No comments:
Post a Comment