Klabu ya Arsenal imepata funzo kutokana na ile ishu ya kuanza kufanya mazungumzo na Alexis Sanchez.
Kuchelewa kulisababisha mgogoro mkubwa baada ya kiungo huyo kuanza mazungumzo na Manchester City.
Sasa imeamua kuanza mazungumzo mapema na wachezaji wake wawili, Aaron Ramsey na Danny Welbeck ili kujadili mkataba mpya.
Wachezaji hao wawili sasa wana miezi 18 iliyobaki katika mkataba wao na mara moja Arsenal imeanza mazungumzo.
Kwa sasa Ramsey analipwa pauni 110, 000 kwa wiki na anaweza kupata hadi pauni 150,000 kwa wiki katika mkataba mpya na Welbeck analipwa pauni 70,000 na mkataba mpya unaweza kumfanya apate hadi pauni 110,000 au zaidi kwa wiki.
No comments:
Post a Comment