KOTEI NI BORA,MKUDE ANASTAHILI: NIYONZIMA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 15 September 2017

KOTEI NI BORA,MKUDE ANASTAHILI: NIYONZIMA

KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima amesema James Kotei ni kiungo bora kucheza kikosi cha kwanza lakini, Jonas Mkude naye anastahili kucheza ‘first eleven’.

Niyonzima, raia wa Rwanda, tangu ajiunge na Simba msimu huu tayari ameshaichezea michezo miwili ya Ligi Kuu Bara, lakini Mkude aliyeongeza mkataba mpya yeye hajacheza hata mechi moja. Kotei raia wa Ghana ndiye amekuwa akitumika katika kiungo cha ukabaji badala ya Mkude.

Akizungumza Niyonzima alisema licha ya Simba kupata matokeo mazuri uwanjani, kukosekana kwa Mkude kunawafanya washindwe kujitawala zaidi mchezoni kutokana na uzoefu alionao. “Mkude ni mchezaji mzoefu kwenye ligi kuu, mbali na hilo pia ndiye mchezaji mzoefu pekee katika kikosi chetu cha sasa na ukiangalia amekuwa kama kiongozi, huyu anaijua timu kwa mambo mengi uwanjani.

“Sijui nini kimekosekana kiasi cha kumfanya ashindwe kucheza kwenye mechi zetu hasa hizi za ligi kwani ninavyomjua mimi amekuwa mahili sana katika nafasi yake uwanjani. “Namjua Mkude kwa muda mrefu sasa, japokuwa nilikuwa Yanga, ila kwa uzoefu wangu naona Kotei (James) ni mzuri ila umuhimu wa kuwa na Mkude katika kikosi cha kwanza bado upo,” alisema Mkude

No comments:

Post a Comment