MASHABIKI WA YANGA,MAJIMAJI WAZICHAPA KAVUKAVU, SONGEA PRESHA TUPU. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 16 September 2017

MASHABIKI WA YANGA,MAJIMAJI WAZICHAPA KAVUKAVU, SONGEA PRESHA TUPU.

Hapa Songea  imekuwa ni presha ya mchezo wa Majimaji dhidi ya Yanga ni kubwa mjini hapa ambapo mashabiki wa timu hizo walikunjana kisha kupigana na kusababisha baa kufungwa usiku wa kuamkia jana.

Mashabiki wa timu hizo usiku huo wakiwa baa, walianza kutambiana kuelekea mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Majimaji na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji.

Kuanzia majira ya saa mbili usiku, mashabiki kadhaa wa Yanga waliotoka Dar es Salaam na wengine wenyeji wa hapa Songea, waliwasili katika baa iliyo jirani na Uwanja wa Majimaji kutakapofanyika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, lakini baadaye mashabiki wa Majimaji nao wakawasili.

Mashabiki wengi wa Yanga wakiwa na jezi zenye
rangi ya njano na kijani, wakiwa wanajitamba kuwa wao ni timu kubwa na lazima watashinda hata kama Majimaji watakuwa wamepania, muda mfupi baadaye mashabiki wa Majimaji waliokuwa wachache nao wakaanza kujibu
mashambulizi kwa tambo.

Majibizano hayo yakasababisha waanze kushikana, kwani wakati huo baadhi yao walikuwa wameshakolea ‘kilaji’, mzozo huo ukawa unaongezeka kila muda.

Kuona hivyo, mwenye baa hiyo licha ya kuwa ilikuwa ni saa tano usiku akaamua kuzima muziki ambao ulionekana kama ‘unawakoleza’ zaidi mashabiki hao, na kuamuru wote kuondoka na baa ikafungwa hata kabla ya muda wake ambao inaonekana siyo kawaida.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao waliahidi kurejea jana kwenye baa hiyo kuendeleza makamuzi kama kawaida wakisubiri mechi hiyo ya aina yake.

No comments:

Post a Comment