KIGOGO WA TSHISHIMBI ATUA MAZOEZINI YANGA,AFANYA KIKAO CHA SIRI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 6 September 2017

KIGOGO WA TSHISHIMBI ATUA MAZOEZINI YANGA,AFANYA KIKAO CHA SIRI.

KATIKA kuhakikisha kikosi cha Yanga kinamaliza tatizo la beki wa kati, mmoja wa wapenzi wa timu hiyo, Shabani Hussein ‘Papaa Ndama’ , jana alifika kwenye mazoezi ya timu hiyo na kufanya kikao cha siri kilichokuwa na ulinzi mkali wa makomandoo na benchi la ufundi kufuatia kutua kwa beki mpya, Fiston Kayembe raia wa DR Congo.
Bosi huyo inadaiwa ndiye aliyekuwa katika mipango ya kumleta kiungo kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi , lakini pia amehusika kumleta Kayembe ambaye ni rafiki mkubwa wa Tshishimbi kwa ajili ya kufanya majaribio.
Ndama alifika kwenye mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar kwa usiri mkubwa kwa lengo la kutaka kumuangalia beki huyo aliyeanza kufanya majaribio hayo ili kuziba nafasi ya beki wa kati, Vincent Bossou raia wa Togo, akitokea katika Klabu ya SM Sanga Balende.
Bosi huyo aliyekuwa ameambatana na mtu mwingine wakiingia uwanjani hapo kisha kukaa kwenye eneo la jukwaa kuu kufuatilia mazoezi hayo kabla ya kufanya kikao cha siri na benchi la ufundi, ambacho kilikuwa na ulinzi mkali wa makomandoo.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, kililihakikishia Championi Jumatano : “Ndama amekuja kwa ajili ya kumuangalia Kayembe kabla ya kuanza harakati za kumsajili ili kuziba pengo la Bossou kwa sababu huyu mchezaji ni rafiki yake na Tshishimbi.
“Unajua hata kuja kwa Tshishimbi jamaa amehusika, sasa alimuuliza kuhusu beki, ndiyo Tshishimbi akamtaja Kayembe kwa kuwa walikuwa pamoja DR Congo kabla ya kutimkia Mbabane Swallows ambako aliuvunja mkataba wake kwa kuununua na kuja Yanga.”
Mara baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo,
Lakini media zilimnasa Bosi huyo akifanya kikao hicho na kocha George Lwandamina akiwa na meneja wa timu, Hafidh Saleh katika eneo la kuegeshea magari nje ya uwanja, kikao hicho kilitumia dakika kumi huku kukiwa na ulinzi mkali wa baadhi ya makomandoo.

No comments:

Post a Comment