MASAU BWIRE WA RUVU SHOOTING ASEMA BADO WANA NAFASI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 6 September 2017

MASAU BWIRE WA RUVU SHOOTING ASEMA BADO WANA NAFASI.

Pamoja na kuanza Ligi Kuu Bara na kipigo cha mabao 7-0, Ruvu Shooting wanaamini wataamka na kuwashangaza wengi.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kikosi chake hakijakata tamaa kwa kuwa kuna mechi nyingi zinakuja na wataamka.
“Nafasi ya kuamka tunayo, tumeteleza tu na kuteleza si kuanguka.
“Tutawashangaza watu kuwa ni sisi, mwalimu ameona makosa anayafanyia kazi. Wachezaji wameona kilichotokea wanajua wanapaswa kufanya nini.
“Ile ni ligi, hivyo tuna nafasi ya kuinuka na kurekebisha makosa yetu na wakati ndiyo huu,” alisema.
Kabla ya mechi dhidi ya Simba, Masau ambaye ni mwalimu kitaaluma alijigamba sana wangeiangusha Simba, lakini mambo yakaenda tofauti.
Mashabiki wengi wa Simba walionekana kuwa tumbo joto kutokana na maneno ya Masau lakini baada ya ushindi huo mnono walimgeuza “babu” yao kwa utani huku wakimshangilia na kupiga naye picha baada ya kumuona.

No comments:

Post a Comment