LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU SIMBA 1-0 MWADUI (KIPINDI CHA PILI.) - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday 17 September 2017

LIVE KUTOKA UWANJA WA UHURU SIMBA 1-0 MWADUI (KIPINDI CHA PILI.)

Dk 52 Manula analazimika kuruka juu kudaka mpira wa krosi wa Ndeule
Dk 51, Okwi anaingia vizuri, anabaki yeye na kipa Massawe anaachia mkwaju mkali kipa anadaka hapa
Dk 48, Okwi anaingia vizuri, anatoa krosi nzuri lakini Ndeule anaokoa vizuri kabisa
Dk 45 Simba wameanza kwa kasi wanaonekana wamepania kupata bao la pili
MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa lakini beki anazuia na kipa anauwahi
Dk 44, mpira zaidi unachezwa katikati ua uwanja
Dk 42, Simba wanapoteza nafasi nzuri kabisa kupitia Gyan ambaye anaonyesha hayuko siriaz
Dk 39, mpira wa adhabu unatua kichwani kwa Kotei lakini anapiga juuuuuu, goal kick
SUB Dk 35 Gerrard Mathias anakwenda nje kwa MWadui, wanamuingiza Benedicto Mwampyate
Dk 30 Okwi anaingia vizuri, mpira unaokolewa na kuwa kona, inachongwa inaokolewa
Dk 26,Bocco tena anaingia na kupiga krosi safi, inaokolewa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya na kipa anadaka kwa ulaini
Dk 25, Bocco anaruka na kupiga kichwa safi cha kuchupa lakini Massawe anauona
Dk 25, Kichuya anaachia mkwaju mkali unagonga mtambaa wa Panya
Dk 24, pasi nzuri ya Kichuya, Gyan anaachia mkwaju wa chinichini lakini kipa Massawe wa Mwadui anadaka vizuri
Dk 21, mwadui FC wanafanya shambulizi mfululizo na Kabunda anaachia shuti tena, lakini hakulenga lango, goal kick
Dk 20, Mwadui FC wanapata faulo nje kidogo ya lango la Simba, Kabunda aliwekewa kigingi
Dk 19, Awadhi Juma anaachia mkwaju lakini unakuwa nyanya hapa
Dk 16, Okwi anapiga shuti la mkwaju wa faulo lakini mpira unapita juuu
Dk 15, Simba wanapata faulo nje kidogo ya lango la Mwadui FC, Okwi alifanyiwa madhambi.
Dk 12 Seseme naye katika nafasi nzuri lakini mpira wake wa krosi unaishia mikononi mwa Manula
Dk 9, Malika Ndeule anaingia vizuri lakini Juuko anaokoa vizuri
GOOOOOOOOO Dk 7, Okwi anafunga bao baada ya kupiga mkwaju wake uliomgonga beki na kujaa wavuni. Alipokea pasi ya Kichuya aliyegongeana naye vizuri
Dk 5 sasa Simba, wanaonekana kupambana na MWadui FC katikati ya uwanja lakini hakuna mashambulizi
Dk 1, Nicholas Gyan naye anaingia vizuri kabisa na kuachia mkwaju lakini inakuwa ni goal kick
Dk 1, Mwadui FC wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Simba lakini shuti lililopigwa linapita juu
KIKOSI CHA SIMBA:
1. Aishi Manula
2. Ally Shomari
3. Mohamed Zimbwe Jr
4. Salim Mbonde
5. Juuko Murshid
6. James Kotei
7. Nicholous Gyan
8. Muzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya
AKIBA:
Emmanuel Mseja
Jamal Mwambeleko
Jonas Mkude
Said Ndemla
Mwinyi Kazimoto
Laudit Mavugo

No comments:

Post a Comment