Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy, amefunguka juu ya video yake ya utupu na rapper Bill Nas ambayo ilisambazwa mitandaoni, na kusema kwamba anafurahi kujua ni jinsi gani wana mapenzi naye ya kweli baada ya kumjia juu.
Nandy amefunguka hayo alipokuwa akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba unapokosea ndipo unajua watu gani wana mapenzi ya kweli na wewe pale wanapokuonya, hivyo amefurahi kuna watu wengi wanaompenda ambao walichukizwa na tukio lake.
“Nimegundua nina watu ambao wananipenda sana kutoka moyoni, unajua mtoto akikosea lazima apewe adhabu, mimi nimefurahi, sio kila mtu atakufuata kukuuliza kwa nini unafanya hivi, ilikuwa ni ngumu kuelewa imetokeaje ila sasa wameanza kuelewa Nandy hakufanya hiyo ilitokea kama inavyowatokeaga watu wengine, so, nimefurahi”, amesema Nandy.
Hivi karibuni msanii huyo alizua gumzo mpaka Bungeni baada ya video yake ya utupu akiwa faragha na Bill Nas kuvuja mitandaoni, kitendo ambacho kilimfanya apitie wakati mgumu hadi kufikia hatua ya kwenda kwa mtaalamu wa saikolojia ili aweze kukaa sawa.
No comments:
Post a Comment