MAMA KANUMBA ALAMBA SHAVU BURUNDI.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 3 May 2018

MAMA KANUMBA ALAMBA SHAVU BURUNDI..

MAMA mzazi wa aliyekuwa staa maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa juzikati ametimkia nchini Burundi kwa mualiko maalum aliopewa na wasanii wa kule ili kujifunza juu ya kazi zao za filamu walizofanya.
 mama Kanumba alisema kuwa baada ya kupata mualiko huo kutokana na wasanii hao kuthamini mchango wa marehemu mwanaye, ameona ni vyema kwenda na kitu nchini humo ambapo ataizindua filamu yake inayoitwa Capten Habona.
“Yani najisikia ni mtu ambaye ninaheshimika ingawa mtoto wangu hayupo hivyo filamu yangu hiyo nitazindulia huko kwa vile na wao wamenipa heshima kubwa sana kwa kuwa filamu yenyewe ina historia nzuri sana,” alisema mama huyo

No comments:

Post a Comment