NDEGE YA TANZANIA IMERUHUSIWA KUONDOKA NCHINI CANADA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 30 March 2018

NDEGE YA TANZANIA IMERUHUSIWA KUONDOKA NCHINI CANADA.

Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dr. John Pombe Magufuli imethibitishia wananchi kuwa ndege aina ya Bombardier Q400 ambayo ilikuwa imezuiliwa nchini  Canada kuondoka imeruhusiwa.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo (Machi 30, 2018) katika ukurasa wake maalumu wa kijamii akiwa ameambatanisha pamoja na picha zilizokuwa zikionesha ndege hizo.
"Ndege yetu aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania pia ndege kubwa nyingine tatu (2 Bombardier CS300 kutoka Canada na  1 Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani) zitawasili baadaye mwaka huu. Nawatakia Ijumaa Kuu njema", amesema Msigwa
Kwa upande mwingine, Msigwa amesema hawajajua tarehe maalumu ya kutua ndege hiyo katika ardhi ya Tanzania kutokana na baadhi ya vitu kuwa vinamaliziwa.

No comments:

Post a Comment