MANARA APIGWA ONYO KALI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 3 May 2018

MANARA APIGWA ONYO KALI.

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amepewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani kushangiklia ushindi wa timu yake mara baada ya mechi kumalizika kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Mtendaji mkuu wa Bodi Ligi Boniface Wambura na kusema uamuzi huo umeafikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichopitia taarifa na matukio mbalimbali ya ligi msimu wa 2017/18 yanayoendelea kulindima hivi sasa ambapo kilibaini tukio la utovu wa kinidhamu kwa afisa huyo.
"Katika mechi namba 178 dhidi ya Yanga SC iliyochezwa Aprili 29, 2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa aliingia uwanjani Haji Manara kushangilia ushindi wa timu yake. Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo, inayozuia wasiohusika kuingia uwanjani kabla, baada na wakati mechi ikiendelea", amesema Wambura.
Aidha, Wambura amesema wametoa adhabu hiyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi kuu Kuhusu Taratibu za Michezo.
Kwa upande mwingine, Wambura amesema endapo Afisa Habari huyo ataendelea na vitendo hivyo vya Kanuni, Kamati itamchukulia hatua kali za kinidhamu dhidi yake. 

No comments:

Post a Comment