Mbowe amesema hayo April 4, 2018 na kudai kuwa kwa sasa hawezi kumlaumu Spika wa Bunge, Job Ndugai bali yeye anamlaumu Katibu huyo wa Bunge kwani amekuwa kikwazo na kusema kuwa hatoweza kuwadhibiti kama ambavyo anafikiri.
"Hatutakubali hotuba za kambi rasmi ya upinzani bungeni ziwasilishwe kwenye ofisi ya Katibu wa Bunge zikafanyiwe 'censorship' ondoa hiki hiki ndiyo, yaani sisi tufanye kazi ya kufanya utafiti tuandike tunachokiamini tuwapelekee wao wakarekebishe wanavyotaka, wao watakavyofanya hivyo hizo hotuba hatutazisoma lakini hatutasusa vikao vya bunge. Tunamwambia Katibu wa Bunge kambi hii kuwepo hapa si fadhila yake bali ofisi ya Kambi Rasmi ya Upinzani ipo kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni za kambi na kanuni za Bunge kama ni mgeni katika Bunge asifikiri hapa kuna mtumishi wake hakuna mtumishi wa Katibu wa Bunge hapa, tunawatumishi wa watu, viongozi wenye akili timamu , wabunge wenye akili timamu walioletwa hapa na wananchi, hawakuletwa hapa na Katibu wa Bunge"alisisitiza Mbowe.
Aidha Mbowe aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo na kusema kwa sasa hawawezi kumlaumu Spika wa Bunge Job Ndugai kwa kuwa alikuwa kwenye matibabu hivyo wanasubiri kuona
"Simhukumu sana Spika wa Bunge kwa sababu alikuwa kwenye matibabu na amerejea amesema Jumanne ya wiki ijayo ataitisha 'commission' namshukuru lakini tunamtaka Spika aelewe kwamba Katibu wa Bunge ni tatizo, huyu yupo hapa kwa ajili ya kuthibiti wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, tunamwambia Katibu hatoweza kutudhibiti" alisisitiza Mbowe
No comments:
Post a Comment