TFF YATOA MAAMUZI HAYA DHIDI YA YONDANI - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 3 May 2018

TFF YATOA MAAMUZI HAYA DHIDI YA YONDANI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetoa maamuzi yake ya awali kwa kumsimamisha mchezaji wa Yanga Kelvin Yondani kutokana na kitendo chake cha kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba SC kwenye mchezo wa namba 178 uliochezwa Aprili 29, 2018.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii leo Mei 03, 2018 jijini Dar es Salaam na kusema Uamuzi huo umeamuliwa baada ya Kikao kilichokaliwa Mei 01, 2018 chini ya Mwenyekiti wake Clement Sanga pindi walipokuwa wanapitia matukio mbalimbali yaliyoweka kujitokeza katika mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amesimamishwa hadi suala lake la kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Adhabu ya kusimamishwa kwake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi", amesema Wambura.
Kitendo cha Kelvin Yondani kumtemea mate mchezaji mwenzake Asante Kwasi katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa 'Kariakoo Derby' kiliweza kuamsha hisia kali kwa wapenda soko nchini, huku wengine wakifika mbali zaidi wakizita mamlaka husika kutolifumbia macho suala hilo kwa madai haliendani na utamaduni wa michezo.

No comments:

Post a Comment