WEMA SEPETU HAWEZI KUWA MKALI KAMA RIYAMA ALLY : MZEE MAJUTO - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 4 April 2018

WEMA SEPETU HAWEZI KUWA MKALI KAMA RIYAMA ALLY : MZEE MAJUTO

Siku chache baada ya kufanyika kwa tuzo za Filamu zinazojulikana kama Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) na mrembo Wema Sepetu kuibuka mshindi kwa upande wa waigizaji wa kike, msanii mkongwe nchini Amri Athumani  ‘Mzee Majuto’ amesema mrembo huyo hawezi kuwa mkali kushinda Riyama Ally.

Katika kipengele hicho Wema alikuwa akichuana na wasanii nane na filamu walizoigiza kwenye mabano akiwemo Getrude Mwita (Bantu), Rachel Kayuga (Safari ya Gwalu), Aisha Mwajumla (Watatu), Riyama Ali (Mama wa Marehemu).

Wengine ni  Amina Rashid (Bandidu), Hawa Abeid (Genge), Sharifa Mansury (Kivuli cha ahadi) na  Neema Mangowi (Malaika) wakati Wema yeye aliingia kupitia filamu yake ya Heven Sent.


Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 4, Mzee Majuto amesema kwake bado Riyama ni mkali na hawezi kufananishwa na Wema katika kuuvaa uhusika anapokuwa mbele ya kamera.

“Mimi nimekaa kwenye fani hii ya uigizaji siku nyingi, najua nani mwigizaji nani amevamia fani japo najua kuna watu wataniponda, lakini ukweli Riyama alistahili kubeba tuzo ile na sio Wema,” amesema msanii huyo anayewavunja watu mbavu kwa vichekesho.

Pia ametaja sababu ambazo ameona ndizo zilizomwezesha Wema kushinda kuwa zimetokana na mambo ya kidijitali, kwa yeye kuwa na mashabiki wengi mtandaoni ambao waliweza kumpigia kura tofauti na wasanii wengine alioshindanishwa nao.



Katika ushauri wake, Mzee Majuto amesema ni vizuri wakati mwingine majaji wasiangalie hilo la upigaji kura na badala yake waangalie vipaji vya watu kwani kwa kufanya hivyo itawavunja moyo wengine wanaotaka kufanya vizuri kwa kuona tayari wana washindi wao mfukoni.



Hata hivyo kwa upande wa msanii bora wa kiume, Mzee Majuto amesema Ahmed Salim ’Gabo’ amestahili kwa kuwa hakuna asiyejua kipaji cha msanii huyo tangu alivyoanza kung’ara kwenye filamu mbalimbali alizoigiza.



Katika tuzo hizo, vipengele 19 vilikuwa vikishindaniwa, ambapo kwa washindi bora wa kike na kiume kila mmoja aliondoka na tuzo na Sh5 milioni taslimu, wakati vipengele vingine walipata Sh1 milioni.

No comments:

Post a Comment