WEMA KUCHUKUA NAFASI YA JOKATE UVCCM..!? - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 4 April 2018

WEMA KUCHUKUA NAFASI YA JOKATE UVCCM..!?

Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James amefunguka juu ya tetesi za sababu ya kutumbuliwa Jokate Mwegelo kwenye umoja huo na kwamba nafasi yake inakusudiwa kuchukuliwa na mlimbwende Wema Sepetu.

Mwenyekiti wa Umoja huo Kheri James amesema kwamba sababu za kutolewa Jokate hawezi kuziweka wazi, lakini si kweli kwamba Wema Sepetu ndiye anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo, kwani hata hivyo hamfahamu Wema Sepetu
Kheri amesema hamfahamu Wema Sepetu zaidi ya kumsoma kwenye magazeti, kwani licha ya kwamba amerudi kwenye chama cha CCM, lakini hajajiunga na umoja huo.
“Wema mimi simjui namsoma tu kwenye magazeti, amerudi CCM lakini si UVCCM, na kama ambavyo hatukuwaeleza sababu za kuteuliwa kwake, ndivyo ambavyo hatutawaambia sababu za kutolewa kwake kwake haina umuhimu sana ya kuwapa watu sababu zake, kwani huenda zinaweza wengine wasifurahie au zikaharibu sifa zake”, amesema Kheri James.
Mwenyekiti huyo wa Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi pia ameelezea kwamba UVCCM ni taasisi ambayo inafanya maamuzi yake kwa kuzingatia, na hawawezi kukurupuka na kufanya umuzi wowote.

No comments:

Post a Comment