HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAE PATA MIMBA KURUDI SHULE KUTOKA KWA MH.DKT.JOHN POMBE MAGUFULI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 23 June 2017

HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAE PATA MIMBA KURUDI SHULE KUTOKA KWA MH.DKT.JOHN POMBE MAGUFULI.

Mh.Dkt.John Pombe Magufuli amewahutubia wakazi wa Bagamoyo mkoani Pwani amesema hakuna mwanafunzi aliye beba ujauzito atarudi shule katika utawala wake.
Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi “ inaweza kufikia kipindi darasa zima lina watoto mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha”.
Hata kama ni mtoto wangu nimekupeleka shule alafu upate mimba nikurudishe ?
Aende akapate mimba aone kama nitamrusisha.
Mimi nimetoa fedha mwanafunzi asome bure halafu leo mtu apate mimba arudi shuleni ndani ya utawala wangu haitatokea.
Wakati mwingine ukisikiliza hizo NGO's zitakuwa zina peleka taifa pabaya kama zinawapenda sana hao watoto zifungue shule zao za kusomesha wazazi serikali haiwezi kuwasomesha.
Ni ziara ya Mh.John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Bagamoyo mkoani Pwani.
                     @erickpicson
   Instagram,Facebook na twitter.

No comments:

Post a Comment