Dar es Salaam. Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba watakuwa na kubarua kigumu Jumamosi mbele ya vinara wenza Mtibwa Sugar katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba na Mtibwa Sugar zote zinapointi 11, wakitofautiana kwa mabao hali inayofanya makocha wa timu hizo kutazama kwa jicho la tofauti mechi hiyo.
Kocha wa Simba, Joseph Omog alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutoka na Mtibwa kuanza vizuri msimu huu tena kikosi chao kikiwa na wachezaji wenye vipaji licha ya kuondokea na wachezaji wao muhimu msimu huu.
Omog alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutoka na timu zote kuwa na pointi sawa licha ya wao kuwa na idadi kubwa ya magoli na timu itakayopata ushindi kwenye mechi hiyo ndio watakuwa vinara wa ligi jambo ambalo litawafanya kutumia nguvu na maarifa ili kushinda.
“Nimewaona Mtibwa wakicheza na Yanga na walicheza vizuri jambo ambalo limenifanya kuwa na maandalizi kwa umakini ili kutumia mapungufu niliyoyaona kwenye hiyo na kuweza kupata matokeo ya ushindi katika mechi ambayo itakuwa na ushindani dakika zote tisini,” alisema Omog.
“Mtibwa ni moja ya timu nzuri inawachezaji wengi wenye vipaji na wameanza vizuri msimu huu, kwahiyo mechi haitakuwa rahisi kabisa ingawa naendelea na maandalizi vizuri na wachezaji wangu ili kuibuka na pointi tatu ambazo tutaendelea kubaki kileleni,” alisema Omog.
Nahodha wa Simba, Method Mwanjali alisema lengo lao msimu huu ni kufanya vizuri katika ligi, lakini haitakuwa kazi rahisi kwani kila timu wanayokutana nayo watakuwa wanakamia ili wachezaji wao kuonyesha kweli wanacheza na Simba kama ilivyokuwa mechi dhidi ya Mbao Fc.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment