PICHA ZA UTUPU NI STAILI ILIYO FELI-TUNDA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 5 September 2017

PICHA ZA UTUPU NI STAILI ILIYO FELI-TUNDA.

Tunda Sebastian.
MUUZA nyago machachari Bongo, Tunda Sebastian amewapa makavu mamodo wanaoibuka kwa staili ya kupiga picha za utupu akisema fasheni hiyo hivi sasa imefeli, hivyo ni bora wakitafuta namna nyingine ya kutoka.
Akipiga stori , Tunda alisema wasichana wanaokuja na kudhani kuwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni kutawafanya wawe maarufu, wamechemsha kwa sababu wanachokifanya ni ujinga uliopitiliza.
“Ninachokiona hapo ni upumbavu tu na tamaa ya umaarufu bila kutafakari madhara yake, kifupi watafute plan B maana A imefeli na kuwadhalilisha,”alisema

1 comment: