BREAKING NEWZ : WATU 12 WAMEFARIKI NA ZAIDI YA 40 KUJERUHIWA KATIKA AJALI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 5 April 2018

BREAKING NEWZ : WATU 12 WAMEFARIKI NA ZAIDI YA 40 KUJERUHIWA KATIKA AJALI.

Watu 12 wamefariki dunia na zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria City Boy kugongana na fuso usiku wa kuamkia leo mkoani Tabora.

Jeshi la Polisi mkoani Tabora limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo dereva wa basi naye ametajwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki, na wahusika wa fuso kukimbia wakilitelekeza fuso hilo, 
Polisi mkoani Tabora wanaendelea kufuatilia idadi ya marehemu kwani inaongezeka na kuangalia majeruhi, na litatoa taarifa zaidi juu ya ajali hiyo baada ya muda mfupi.
Endelea kubaki nasi kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment