Mama mzazi wa msanii Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo amefariki dunia.
Bi. Mbibo amefariki alfajiri ya leo Aprili 26, 2018 akiwa nyumbani kwake Jet, Dar es Salaam.
Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema mama yao amefariki mara baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.
April 01, 2018 Lady Jaydee alizungumza kuhusu kuugua kwa mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;
Nauguza mama mzazi lakini naendelea kupambana na maisha vilevile, usinione naimba au natabasamu ukafikiri nina raha sana.
Sina raha wala nini, lakini pia lazima nifanye kazi ili niweze kuishi, bila kuangalia kama watu watani judge vipi!, Kwani bado naamini Mungu atamponya na kumnyanyua kwenye kitanda alicholala kwa zaidi ya miezi 2, Kwani Mungu pekee ndio anaeweza.
Bi. Mbibo alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo alipatiwa matibabu hapa nchini na nje ya nchini (India).
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet, Dar es Salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika
No comments:
Post a Comment